Kiswahili lugha yangu, tamu kuliko zote;
Nilofunzwa na mamangu, nilipoanza kumwaga nyute;
Yavutia moyo wangu, naisifu kote kote;
Kiswahili lugha tamu, asali mtoto wake.
Napenda zako hadithi, na yako mashairi;
Mafumbo, methali, navyo vitendawili;
Ungekuwa chanda changu, ningalikuvika pete;
Wakujue walimwengu, watake wasitake;
Wewe si tam’-chungu, bali kipenda mate;
Kiswahili lugha tamu, asali mtoto wake.