Nimeamua kuipaza , hii mbiu ya mgambo;
Nashindwa kunyamaza, lanikera hili jambo;
Nawazua nikiwaza, fumbueni hili fumbo;
U’socialite’ ni nini? Nimwelezeje wangu binti?
Naomba usaidizi, kuielewa hii kazi;
Shahada yao ni ipi, yapatikana chuo kipi?
Masomo yao ni yepi, n’elezeni (tu) kwa ufupi;
U’socialite’ ni nini? Nimwelezeje wangu binti?