Mabilionea wa korona, mwingine ka nyie hakuna;
Hata haya hamna, msichopanda mwavuna;
Raha gani mwaona, kujifaidi na hili janga;
Zitawafata laana, mwacheza na Maulana.
Wauguzi taabani, mganga yu mashakani;
Watupe vipi huduma, na PPE hamna?
Maisha yao hatarini, na hata bima hawana;
Mshahara Je? Duni Malipo ni kuvurutana.