Mabilionea wa korona, mwingine ka nyie hakuna; Hata haya hamna, msichopanda mwavuna; Raha gani mwaona, kujifaidi na hili janga; Zitawafata laana, mwacheza na Maulana. Wauguzi taabani, mganga yu mashakani; Watupe vipi huduma, na PPE hamna? Maisha yao hatarini, na hata bima hawana; Mshahara Je? Duni Malipo ni kuvurutana.