Nimeamua kuipaza , hii mbiu ya mgambo; Nashindwa kunyamaza, lanikera hili jambo; Nawazua nikiwaza, fumbueni hili fumbo; U’socialite’ ni nini? Nimwelezeje wangu binti? Naomba usaidizi, kuielewa hii kazi; Shahada yao ni ipi, yapatikana chuo kipi? Masomo yao ni yepi, n’elezeni (tu) kwa ufupi; U’socialite’ ni nini? Nimwelezeje wangu binti?